Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchumi kuporomoka kwa 3.8%

Mwigulu Uchumi Kupungua.png Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Mwaka 2021, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zilikuwa na ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia 4.5, ikilinganishwa na ukuaji hasi wa asilimia 1.7 mwaka 2020.

Hii ilitokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa ili kuimarisha ukuaji wa uchumi ikiwemo kuboresha huduma za afya pamoja na kuimarika kwa bei za bidhaa zinazouzwa nje ya ukanda huo baada ya kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa UVIKO-19.

Ukuaji wa uchumi katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua na kufikia wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2022 na utaongezeka kufika wastani wa asilimia 4.0 mwaka 2023.” Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/2023

Chanzo: www.tanzaniaweb.live