Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchimbaji madini, kilimo cha tumbaku vyatajwa chanzo cha uharibifu wa mazingira

Kero Madini Uchimbaji madini, kilimo cha tumbaku vyatajwa chanzo cha uharibifu wa mazingira

Mon, 6 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchimbaji wa madini ya dhahabu na kilimo cha tumbaku katika halimashauri ya Wilaya ya Chunya vimetajwa kuwa ni baadhi ya shughuli kuu zinazochangia uharibifu wa mazingira wilayani hapa.

Sababu hizo zimebainishwa leo Juni 5, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka Mayeka alipokuwa akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kimkoa imefanyika wilayani Chunya.

Mayeka amesema Serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kila wanapokuwa na mihadhara ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu ambapo amesema hali hiyo ikifumbiwa macho itasababisha wilaya kugeuka kuwa jangwa.

Amesema wachimbaji wa madini wamekuwa wakitumia kemikali ya zebaki kwenye maeneo ya mito na vyanzo vya maji na wakulima wa tumbaku hufyeka misitu ovyo kwaajili ya kukaushia tumbaku hali hiyo amedai inaweza kusababisha ukosefu wa mvua na kuharibu vyanzo vya maji.

Awali Kaimu Katibu Tawala Msaidizi (uchumi) Mkoa wa Mbeya Said Madito  amesema kila mwaka wanatakiwa kupanda miti 10.5 milioni na kwa kila wilaya inatakiwa  kupanda miti 1.5 milioni ili kurejesha hali ya  uharibifu wa mazingira.

Madito amesema kumekuwa na changamoto ya ya utunzaji wa miti hiyo inayoyopandwa hata hiyo katika Mkoa wa Mbeya kwa miaka miwili mfululizo 2020-2021 walipanda miti 7.29 milioni sawa na asilimia 67 na 2021-2022 walipanda miti 7.49 milioni.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya Noel Chiwanga amesema shughuli zinazoharibu mazingira ukiacha uchimbaji wa madini ya dhahabu ni ufugaji wa kuhama kuhama.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema shughuli za utafutaji madini ya dhahabu wilayani Chunya zimekuwa zikiharibu mazingira kwa kuwa baadhi ya watu huingia hadi kwenye maeneo ya barabara kuchimba hali inayoharibu miundombinu.

Mkazi wa mamlaka ya mji mdogo Makongolosi Richard Nguge amesema Serikali ina wajibu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na kasi ya uharibifu wa mazingira ilivyo katika maeneo mengi yanayochimbwa dhahabu.

Hata hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya yalipofanyika maazimisho hayo kimkoa  amesema Serikali itaendelea kuzimamia sheria na kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira hivyo na kuwataka watendaji wa vijiji kuwahimiza wananchi kufuata sheria badala ya kuharibu mazingira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live