Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchenjuaji madini chanzo cha kukosekana maji safi

6aaa911fc211b4c8e0f62459385c1104 Uchenjuaji madini chanzo cha kukosekana maji safi

Sat, 28 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

S HUGHULI za uchimbaji na uchenjuaji wa madini wilayani Geita mkoani hapa zimeelezwa kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa vyanzo vya maji hali inayopelekea uhaba wa huduma ya maji safi na salama kwenye baadhi ya maeneo.

Hayo yamebainishwa juzi na Ofisa wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilayani Geita, Benjamin Mtatwa wakati wa mkutano wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika na wadau wa maji wilayani hapa. Mtatwa alisema baadhi ya wachimbaji wadogo wanafanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji na hata kuchepusha mito kuelekea maeneo yao kwa ajili ya shughuli za uchenjuaji na hivyo kuathiri kiwango na usalama wa maji.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Bonde la Maji ya Ziwa Tanganyika, Odemba Cornel alieleza miongoni mwa vyanzo vya maji vilivyoathirika kwa kiwango kikubwa ni mto Nikonga ambapo kiwango cha maji kimepungua na maji siyo salama.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Geita na Ofisa Tawala wa Wilaya, Fred Muhagama alikiri tatizo hilo lipo na kuwataka viongozi wa ofisi za vijiji na kata kuimarisha usimamizi wa vyanzo vya maji na kudhibiti matumizi holela ya maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live