Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubovu miundombinu kaa la moto Bandari ya Karema

Bandari Karema (600 X 346) Ubovu miundombinu kaa la moto Bandari ya Karema

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imetaka juhudu za haraka kufanyika kurekebisha miundombinu ya barabara na reli kutoka Mpanda hadi Bandari ya Karema wilayani Tanganyika ili kuiwezesha bandari hiyo kufanyakazi.

Bandari hiyo iliyogharimu Sh bilioni 47.97 wakati wa ujenzi ilifunguliwa Septemba 2022 lakini imeweza kutengeneza kiasi cha Sh milioni 4.8 tu.

Mwenyekiti wa Kamati, Jerry Silaa amesema ubovu wa miundombinu umeathiri utendaji wa bandari hiyo muhimu inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

"Tatizo kubwa la Bandari ile ni barabara, mizigo kufika na kutoka pale, barabara na reli, iko reli ya Kati inafika mpaka Mpanda na umbali wa kilomita 130 kufika mpaka Karema ambazo hazijajengwa na wakati wote serikali imekuwa ikilisema jambo hili," amesema na kuongeza.

"Barabara tuliyoenda, kufika hata gari ndogo ni tabu, Bandari ile inaweza ikapunguza msongamano Tunduma. Leo mizigo ya Congo malori yanatumia siku 45 maana yavuke Tunduma, yaingie Zambia, yaende tena yakavuke kweye mpaka mwingine wa Zambia ndio yanaingia Congo."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live