Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uagizaji wa sukari mwisho 2025

Sukarii Sukari Leseni Uagizaji wa sukari mwisho 2025

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Sukari nchini Tanzania imesema jitihada zinazofanyika za upanuzi na uanzishaji wa viwanda vya uzalishaji wa sukari, vitawezesha kufikia tani 756,000 ifikapo mwaka 2025 hivyo kuondokana na uagizaji wa sukari kawaida.

Hayo yamesemwa jana Jumanne Oktoba 25, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo Profesa Kenneth Bangesi wakati kueleza utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Profesa Bangesi amesema mahitaji ya sukari ya kawaida nchini hadi kufikia Juni 30, 2022 mwaka huu ni tani 645,000 ambapo kati ya hizo tani 440,000 ni za kawaida na tani 205,000 ni za viwandani.

Amesema hadi sasa uzalishaji wa sukari ya viwandani haujaanza nchini na kwamba uzalishaji huo ulichelewa kutokana na soko la mahitaji ya sukari ya kawaida kuwa kubwa sana nchini.

“Hali ya uzalishaji iliyopo hivi sasa, kwa mwaka jana tulizalisha tani 379,000 na hivyo iliacha pengo la tani 60,000 ambayo ilitakiwa kuagizwa kuziba pengo hilo la sukari nchini,” amesema.

Amesema kwa takwimu hiyo upungufu kwa sukari ya kawaida ni tani 60,000 wakati kwa sukari ya viwandani ni tani 205000.

Profesa Bangesi amesema uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka kutoka tani 110,000 mwaka 2004 hadi 380,000 hadi kufikia Juni 30 mwaka huu. Amesema uagizaji huo wa sukari ulikuwa unagharimu zaidi ya Sh300 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live