Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

USAID yafanya kwenye miradi ya bahari

Pic Fedha Data Wastaafu USAID yafanya kwenye miradi ya bahari

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIKA kuhakikisha uchumi wa bluu nchini unazidi kukua, Shirika la misadaa la Marekani ‘USAID’, limetangaza kuiongeza fedha Tanzania katika mradi wa Heshimu Bahari kutoka Dola za Marekani milioni 13 hadi Dola milioni 25 sawa na Sh bilioni 62.525.

Mkurugenzi wa Misheni wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania, Craig Hart ametangaza uamuzi wa kuongeza fedha hizo leo Oktoba 26, 2023 katika Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) yaliyofanyika katika ukumbi wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Amesema nyongeza hiyo imetokana na mazungumzo ya Balozi wa Marekani na Wizara ya Uchumi wa Buluu ya Zanzibar na Wizara ya Mifugo ya Tanzania Bara, yaliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu.

Amesema fedha hiyo itaongeza maeneo ya mradi huo kuhakikisha ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za uvuvi na utunzaji wa rasilimali za bahari.

Maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni Mwambao wa Bahari ya Hindi Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, Mafia, Kilwa na Mnazi Bay Ruvuma.

Amesema mradi huo wa ‘Heshimu Bahari’ ni wa miaka mitano unakwenda kuisaidia Tanzania katika maendeleo ya uchumi wa bluu. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live