Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNCTAD: Afrika inaweza kuwa kiungo muhimu katika usambazaji bidhaa duniani

Bidhaa Afrika Afrikaaa UNCTAD: Afrika inaweza kuwa kiungo muhimu katika usambazaji bidhaa duniani

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi za Kiafrika zinaweza kuwa washiriki wakuu katika mzunguko wa ugavi wa bidhaa duniani kwa kutumia rasilimali zao kubwa za nyenzo zinazohitajika na sekta za teknolojia ya juu na soko lao la wateja linalokua. Hayo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kuhusu Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika mwaka 2023 iliyozinduliwa Jumatano jijini Nairobi, Kenya.

Afisa Mchumi Mkuu wa UNCTAD ambaye pia ameongoza katika kuandika ripoti hii, Habiba Ben Barka anasema Ripoti ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika ya mwaka 2023 inaangalia mikakati, sera, na taratibu tofauti ambazo Nchi za Afrika zinaweza kuweka ili kuunganisha baadhi ya mzunguko huo wa ugavi.”

Mzunguko wa ugavi wa bidhaa unajumuisha mifumo na rasilimali zinazohitajika kuendeleza, kuzalisha na kusafirisha bidhaa na huduma kutoka kwa wasambazaji hadi kwa wateja.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UNCTAD Rebeca Grynspan amesema, "Huu ni wakati wa Afrika kuimarisha nafasi yake katika mizunguko ya ugavi duniani huku juhudi za usambazaji bidhaa zikiendelea. Pia ni fursa kwa bara la Afrika kuimarisha viwanda vinavyoibuka, kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa mamilioni ya watu wake."

Wingi wa madini na vyuma muhimu barani Afrika, zikiwemo alumini, kobalti, shaba, lithiamu na manganisi, vipengele muhimu katika tasnia zinazotumia teknolojia kubwa, vinaliweka bara hili kama kivutio kwa viwanda, kwa sababu misukosuko ya hivi karibuni iliyosababishwa na mtikisiko wa biashara, matukio ya kijiografia na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi zinalazimisha wazalishaji kugawanya maeneo yao ya uzalishaji.

Afrika pia inatoa faida kama vile ufikiaji mfupi na rahisi zaidi wa pembejeo za msingi, nguvu kazi ya vijana inayofahamu teknolojia, na inayoweza kubadilika, na tabaka la kati linalokua na linalojulikana kwa kuendelea kuhitaji bidhaa na huduma za hali ya juu zaidi.

Ripoti hiyo inasema biashara ndogo ndogo na za kati za Kiafrika zinahitaji fedha zaidi za ugavi, ambazo zitaziba pengo la muda wa malipo kati ya wanunuzi na wauzaji, zitaboresha upatikanaji wa mitaji ya kufanya kazi na kupunguza matatizo ya kifedha.

Kulingana na ripoti hiyo, thamani ya kifedha ya soko la ugavi barani Afrika ilipanda kwa asilimia 40 kati ya mwaka 2021 na 2022, na kufika dola bilioni 41.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live