Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UDSM watengeneza mkate, biskuti za senene

Mkate.jpeg UDSM watengeneza mkate, biskuti za senene

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: Habarileo

Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), imeongeza thamani ya mdudu aina ya senene kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo mkate na biskutit kwa kuweka unga wa mdudu huyo.

Mkufunzi Msaidizi kutoka UDSM, Crispin Dionice amesema hayo alipozungumza kuhusu idara hiyo kuongezea thamani ya mazao ya kilimo ikiwa ni pamoja na vyakula vyenye protini.

Amesema wameongezea thamani senene kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa sababu watu hushindwa kumla mdudu huyo lakini kupitia bidhaa kama mkate ama biscuit huweza kula kwa kuwa hawamwoni.

“Yote haya tunayafanya kwa sababu tunatamani hivi virutubisho vilivyopo kwenye senene vifikie kila mmoja, anaweza akala chakula chochote ambacho kimechanganywa na unga wa senene.

“Senene ni mdudu ambaye ana protini kwa wingi, ana mafuta yenye afya tunasema mafuta omega 3 , omega 6 fats acid, mafuta haya ni mazuri kwa ajili ya afya ya moyo, lakini pia ni mazuri kwa ajili ya kujenga afya bora ya ubongo kwa mtoto hata kwa mtu mzima kuweza kuweka sawa kumbukumbu.

“Lakini pia mdudu huyu anayo madini mbalimbali ikiwa pamoja na madini chuma, zink , vitamin b12,” amesema.

Amesema watu wanapata changamoto kumla mdudu huyo ndio maana wakaona watengeneze bidhaa mbalimbali ziweze kuwafikia wengi.

Amesema baada ya kumchakata senene na kupata mafuta, makapi yake huyasaga na kuweza kuchanganywa kwenye bidhaa mbalimbali.

Alisema lengo la kufanya hayo yote ni kuongeza thamani ya mdudu huyo ikiwa ni pamoja na kupunguza tatizo la utapiamlo hapa nchini.

Chanzo: Habarileo