Dar es Salaam. Umewahi kufikiria jinsi ya kuhifadhi juisi ya miwa ambayo inapaswa ikikamuliwa inywewe muda huohuo kwani ikikaa muda mrefu inapoteza ladha yake.
Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania imelifikiria hilo na kuja na mbinu mpya ya kuitunza kwa zaidi ya mwezi mmoja na ikawa na ladha yaje ileile kwenye maonyesho ya 43 ya kimataifa yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwanafunzi wa shahada ya umahiri kutokana idara ya chakula na sayansi wa UDSM Boniface Joshua amesema alifikiria ni kwa namna gani anaweza kutunza juisi ya miwa.
Amesema baada ya kutafakari kwa kina na kukaa maabara kujaribu hiki na kile akabaini akichanganya kitunguu maji na majani ya mti wa mlonge vina wingi wa vihifadhi chakula.
Amesema kwa kutumia vyakula hivyo ameweza kurefusha muda wa kukaa juisi ya miwa kutokana siku sifuri hadi zaidi ya siku 30.
Amesema pia wakati anatafiti alibaini juisi ya miwa inayotengenezwa mtaani ina upungufu wa viini lishe kama vitamini A na C na haina baadhi ya madini muhimu katika mwili wa binadamu kama zink ambayo ni muhimu kwa afya ya uzazi, China, potasiam na sodiam.
Pia Soma
- Takukuru yabaini kasoro miradi ya maendeleo Ilala
- Mwili wa mzamiaji wa ndege kutoka Kenya waanguka ikitua London
- Askofu Kasala akitaka chuo cha Saut kujitathimini
Huku akionyesha juisi ya miwa iliyopo ndani ya chupa ukiwa imefungwa vema amesema kuwa hata ikitingishwa haitoki povu kwa kuwa ipo salama.