Dar es Salaam. Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) idara ya sheria kimeingia mkataba wa makubaliano na Chuo Kikuu cha Zejiang Normal kushirikiana kufanya tafiti za kisheria, kubadilishana wataalamu na wanafunzi.
Akizungumza leo Alhamisi Mei 30, 2019 mkuu wa idara ya sheria binafsi katika shule kuu ya sheria ya UDSM, Dk James Jesse amesema makubaliano hayo yataboresha utendaji wa idara hiyo hasa kupitia tafiti zitakazokuwa zikifanywa.
Amesema katika mkataba huo kutakuwa na kubadilishana wanafunzi wa vyuo hivyo, jambo ambalo ni fursa kwa baadhi ya wanafunzi kutoka Tanzania kwenda kupata mafunzo ya muda mfupi China au kusoma masomo yao.
“Lakini si wanafunzi tu hata walimu wetu watakuwa wakienda kufundisha China na walimu wao kuja Tanzania kufundisha kwetu,” amesema Jesse.
Makamu wa rais wa chuo kikuu cha Zhejing Normal, G?o jù Huí amesema kusainiwa kwa mkataba huo ni mwendelezo wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika kukuza sekta ya elimu.
“Hii itakuwa ni fursa kwa wataalamu wa Tanzania kushiriki kufanya tafiti kubwa za kimataifa na zinazotambuliwa duniani jambo ambalo litawatambulisha,” amesema