Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twitter yawatimua kazi Mameneja wawili kupisha utawala wa Elon Musk

Ellon Mkl Twitter yawatimua kazi Mameneja wawili kupisha utawala wa Elon Musk

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMPUNI YA TWITTER imewatimua kazi Mameneja wawili wa ngazi ya juu na kusitisha ajira ikiwa ni mpango wake wa mabadiliko chini ya utawala mpya wa bilionea namba moja duniani Elon Musk.

Mtandao huo wa kijamii umethibitisha kuondoka kwa Meneja Mkuu Kayvon Beykpour na Mkuu wa bidhaa na kodi Bruce Falck na kusisitiza kuwa ajira itauwa ni kwenye maeneo muhimu tu huku ikisubiri kipindi cha mabadiliko chini ya utawala wa Elon Musk.

Wote wawili walithibitisha kuwa wameondolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Twitter Parag Agrawal.

“Parag aliniambia niondoke baada ya kunijulisha kuwa anataka kuipeleka timu katika uelekeo mwingine.” Alituma ujumbe huo Beykpour kupitia mtandao wa Twiiter na kuongeza kuwa wakati anatimuliwa kazi alikuwa katika likizo ya uzazi.

Nafasi ya Agrawal mwenyewe ipo katika hatari kubwa ya kuchukuliwa na Elon Musk ambaye ni mmiliki mpya wa Twitter, hisa za kampuni hiuo zilishuka kwa 3% siku ya alhamis na kusababisha hasara ya dola milioni 10.

Elon Musk amerudia mara kwa mara kuthibitisha adhima yake ya kuitaka Twitter kuwa jukwaa la uhuru wa kujieleza na kupunguza utegemezi wa matangazo ya biashara kama njia ya kuendesha na kuingiza mapato ya kampuni hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live