Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuzo za walaji zazinduliwa, kampuni 70 kushindana

Trophy Award Ceremony Feat Tuzo za walaji zazinduliwa, kampuni 70 kushindana

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika sehemu ya kusaidia walaji kutoa maoni yao juu ya ubora wa bidhaa na huduma wanazozipata sokoni, tuzo za Consumer Choice Awards Africa (CCAA) 2023 zinatarajia kushindanisha kampuni mbalimbali kwenye aina zaidi ya 70.

Tuzo hizo zinazotokana na Chaguo la Wateja Tanzania zilianzishwa mwaka 2019 chini ya Shirika la Lavine International Agency Limited zinazolenga kutambua na kukuza ubora wa biashara kupitia uchaguzi wa watumiaji na kura zinapigwa kwa mfumo wa dijitali.

Akizungumza katika uzinduzi wa tuzo za mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa CCAA, Diana Laizer alisema mashindano hayo yatahusisha aina kuu 22 za tuzo pamoja na nyingine ndogondogo zaidi ya 70.

Alitaja aina za tuzo zitakazoshindaniwa ni pamoja na usafirishaji, mawasiliano ya simu, usafiri wa anga, huduma za kifedha, ujenzi, huduma za bima, mafuta na gesi, hoteli , usalama, bidhaa zinaotoka haraka, matukio na Mapambo, Mitindo na Ubunifu, pamoja na Upigaji picha.

“Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, tumeweza kufikia maelfu ya wateja barani Afrika kupitia njia ya mtandao na kukusanya maoni yao juu ya bidhaa na huduma wanazotumia na zaidi ya tuzo 70 zimekuwa zikitolewa kila mwaka. Tunajivunia mafanikio haya,” alisema

Akizungumzia mchakato wa kuwapata washindi, Diana alibainisha washindi wa tuzo hupatikana kupitia utaratibu wa kupiga kura mtandaoni ambapo walaji wana nafasi ya kupigia kura bidhaa au huduma mbali mbali zinazoshindanishwa kupitia tovuti ya CCAA.

"Baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwa washiriki katika makundi tofauti, timu yetu inafanya kazi ya kupanga makundi hayo kulingana na mapendekezo na vigezo vya tuzo husika,” alisema

Alisema shughuli hiyo ikikamilika makundi huwekwa mtandaoni na walaji huweza kupiga kura kulingana machaguo yao ambapo upigaji kura hufanyika kwa siku 25 na mlaji anapiga kura mara moja tu katika kila aina ya tuzo.

Kwa mujibu wa Diana, baada ya muda wa kupiga kura kumalizika, mfumo huonyesha matokea kulingana na idadi ya kura ambazo bidhaa au huduma imepigiwa.

“Dirisha la kupendekeza aina za tuzo kwa mwaka 2023 limefunguliwa rasmi kuanzia Juni 18, 2023 na litaendelea hadi Julai 9, 2023. Shughuli ya upigaji kura itatangazwa baadaye mwaka huu kwa hivyo tunahimiza kampuni na chapa kushiriki na kushirikisha wateja wao,” aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live