Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunahitaji takwimu sahihi sekta ya mifugo

Malisho Mifugo Ngombe Tunahitaji takwimu sahihi sekta ya mifugo

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Shamata Shaame amewataka wataalam wa sekta ya mifugo na uvuvi kuhakikisha wanakusanya takwimu sahihi wakati wa kukusanya taarifa za kitafiti ili ziweze kuisaidia serikali kupanga mipango yake.

Waziri Shaame ametoa agizo hilo wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika mkoani Arusha.

“Wizara na wadau wa kilimo, mifugo na uvuvi kwa pamoja lazima tutambue kuwa huu ni wakati mwafaka wa kufanya mapinduzi makubwa katika minyororo ya thamani ya mifugo na samaki ili kukidhi mahitaji ya chakula na lishe bora kwa wananchi na masoko yanayotuzunguka,” amesema Shaame.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi amewataka wataalam kuweka bidii katika kujiendeleza kitaaluma ili kuongeza ujuzi na ufanisi zaidi katika kazi zao na kuweza kutengeneza mfumo utakaohifadhi taarifa za wataalam wote wa mifugo nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live