Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume yajipanga kukusanya bil 600 za madini

D9feb2a7af25bb39d9d7d13a2f973a48 Tume yajipanga kukusanya bil 600 za madini

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAIMU Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, i Yahya Samamba amesema tume hiyo imeweka mikakati ya kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye sekta ya madini ili iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Samamba aliyasema hayo jana Dar es Salaam katika kikao kati ya Tume ya Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikichokua na lengo la kuangalia namna ya utekelezaji wa makubaliano yaliyosainiwa Septemba mwaka jana kuhusu utendaji kazi kati ya TRA na tume hiyo kwenye sekta ya madini.

Samamba alisema ushirikiano kati ya Tume ya Madini na TRA utarahisisha usimamizi kwenye Sekta ya Madini hususan kwenye ukusanyaji wa maduhuli kwa kubadilishana taarifa za kodi mbalimbali zinazolipwa Serikalini.

Kuhusu ukusanyaji maduhuli kwa mwaka wa fedha 2021-2022, mhandisi Samamba alisema tume imeweka lengo la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 600.

Alisema, lengo ni kuhakikisha mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa unakua na kufikia asilima 10 ifikapo mwaka 2025.

Alimshukuru Waziri wa Madini, Doto Biteko, Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kwa msaada kwenye utatuzi wa changamoto.

Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki alisema tangu kuanzishwa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini Machi, 2019 serikali ilipata shilingi bilioni 211.2 za mrabaha na kodi ya ukaguzi kupitia masoko hayo.

Kasiki alisema, ukusanyaji wa maduhuli imeendelea kuimarika nchini kwa kuwa wachimbaji wadogo wa madini wameanza kuwa na uelewa wa umuhimu wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz