Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya Taifa ya umwagiliaji yataka wakulima walipe ada

Kilimo (1) Tume ya Taifa ya umwagiliaji yataka wakulima walipe ada

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvomero. Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetoa elimu kwa wanachama wa ushirika wa wakulima wa mpunga skimu ya umwagiliaji Dakawa (Uwawakuda) iliyopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro kuhusu umuhimu wa uchangiaji wa ada na usajili wa vyama vya umwagiliaji.

Elimu hiyo imetolewa kupitia mkutano wa kawaida wa mwaka wa ushirika huo baada ya wakulima hao kuomba ufafanuzi Kwa tume hiyo Ili waweze kupata uelewa kuhusu sheria ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo inayomtaka mkulima kuchangia ada ya huduma za umwagiliaji na pia kukitaka chama kusajiliwa chini ya tume hiyo.

Akitoa elimu hiyo Ofisa kilimo tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Petro Sarwat ameeleza umuhimu wa uchangiaji ada ya huduma za umwagiliaji ni kuwa ada hiyo itasaidia kuboresha na kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji nchini.

"Moja kati ya vipengele ambavyo tunawaelimisha wakulima wetu waelewe kwamba miundombinu iliyopo ni ya kwao na pia wachangie ili serikali iweze kufikia malengo yake.

“Kwani kwa sasa eneo linalofaa kwa umwagiliaji kwa nchi nzima ni hekta milioni 29 na eneo lililoendelezwa ni hekta 727,280 hivyo Serikali ina majukumu, hivyo wakulima wana wajibu wa kuchangia ili serikali iweze kuboresha miundombinu iliyopo na kuiendeleza," amesema Sarwat.

Kwa upande wake Mhandisi wa umwagiliaji mkoa wa Morogoro, Mohamed Mcheni amesema skimu ya Dakawa ni miongoni mwa skimu kubwa katika mkoa huo, ambapo takribani Sh23.4 bilioni zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo uzalishaji wake ni zaidi ya gunia 20 kwa ekari moja.

"Eneo hili la Dakawa zipo hekta 1,000 ambazo hazijaendelezwa ila zipo kwenye mpango wa mwaka huu wa fedha kufanya upembuzi yakinifu wa kina pamoja na kufanyia usanifu na tutazijenga hizo ambapo kukamilika kwake kutakuwa na hekari takribani 8,000 zitatosha kuzalisha chakula cha kutosha," amesema Mcheni.

Kwa upande wake Ofisa sheria Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Magreth Shayo ametoa wito kwa wakulima wa skimu ya Dakawa na wakulima wote nchini kushirikiana na tume hiyo ili kusaidia kukuza sekta ya umwagiliaji nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live