Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya Taifa ya umwagiliaji yaleta matumaini

Umeagiliajiiiii Timerr.jpeg Tume ya Taifa ya umwagiliaji yaleta matumaini

Fri, 15 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema ziara ya tume ya Taifa ya umwagiliaji katika Mkoa huo italeta tija kwenye kilimo cha umwagiliaji baada ya mwaka huu uzalishaji wa chakula kushuka kulinganisha na mwaka jana.

Homera amesema hayo wakati tume ya Taifa ya uwagiliaji chini ya Mkurugenzi wake, Raymond Mdolwa alipokuwa akitoa taarifa ya ziara yake iliyojumuisha Wizara ya fedha na mipango na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora katika Mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya.

Homera amesema mwaka huu hali ya uzalishaji wa chakula imekuwa ndogo kulinganisha na mwaka jana, huku changamoto ikiwa ni umwagiliaji na kwamba kupitia ziara ya Tume hiyo italeta mabadiliko.

Amesema tume hiyo imetembelea miradi 13 mkoani Mbeya, ambayo inatarajiwa kujengwa ambapo 11 ni ya Wilaya ya Mbarari na mmoja ni Kyela katika skimu ya makwale yenye hekta 2500 na nyingine ya Halmashauri ya Busokelo (skimu ya ya Mbaka yenye hekta 300).

“Kwa maana hiyo tunatarajia kuona uzalishaji wa chakula ukiongezeka baada ya miradi hii kukamilika, niwaombe wananchi na wakulima kwa ujumla kujiandaa na kilimo chenye tija,” amesema Homera.

Kwa upande wake Mdolwa ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo, amesema Mkoa wa Mbeya ili uweze kupiga hatua zaidi kwenye kilimo lazima ujengewe mabwawa ya maji kuliko kutegemea mito.

Alisema kutokana na hali hiyo tayari tume imewaelekeza wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutenga maeneo ambayo yatajengwa zaidi ya mabwa matano ili kumsaidia mkulima kufanya shughuli zake za kilimo.

“Tunaishukuru serikali imetenga Sh 416 bilioni katika idara hii, tunaamini utekelezaji wa miradi hii itakuwa yenye tija ili kuongeza ufanisi kwa mkulima kufanya shughuli zake, niwaombe kujiandaa,” amesema Mdolwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live