Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tsh. Mil. 300/- leseni za biashara zayeyuka

Fedha Wagawana Tsh. Mil. 300/- leseni za biashara zayeyuka

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya shilingi milioni 300 zinazotokana na malipo ya leseni Wilayani Bukoba, mkoani Kagera zimetajwa kutoonekana kwenye mfumo wa mapto mkoani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Moses Machali, alibainisha hayo jana wakati akizungumzia taratibu na mabadiliko ya ukataji wa leseni kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Bukoba.

Machali alisema hali hiyo imelazimu kuunda kamati ya kwenda kufanya msako wa leseni ambazo zimelipiwa na kutoonekana katika mfumo kupitia  maduka na maeneo ya biashara.

"Lakini ninapoongea hapa, tayari kuna kamati itaanza kesho itakayopita duka kwa duka kujiridhisha na leseni zilizoko na zilizofanya kuonekana kuna malipo lakini pesa hazipo," alisema Machali.

Alisema wafanyabiashara wanafika kulipia ada ya leseni na kuacha pesa lakini haifiki serikalini badala yake kuingizwa mfukoni.

"Mfano mimi ndiye nakata leseni unakuta natengeneza namba A malipo yenye Sh. 100,000 hiyo ni upande wa serikali lakini mteja ametoa Sh. 300,000, Sh. 200,000 zote nakunja naweka mfukoni," alisema Machali.

Alisema mfanyabiashara akija kuchukua leseni kwa sababu kile ni kitabu atachaniwa na kupewa karatasi ya Sh. 300,000 na hajui aliyolipa halali ni Sh. 100,000.

Machali alisema vitendo hivyo vinafanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kazini na kusababisha serikali kukosa mapato ya kuendesha miradi yake.

Mkurugenzi wa  Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu, alisema usajili wa mfumo hufanya kutambua aina ya biashara inayofanywa na mhusika na kufuatilia malipo anayostahili kulipa.

Njovu alisema endapo mfanyabishara amemaliza malipo yake, anatakiwa apewe stakabadhi inayoonyesha malipo na kiasi cha pesa aliyotoa kabla hajapokea leseni aliyokata.

Hata hivyo, alisema leseni ina hatua tano  ambazo ni uombaji wa kuwa  na biashara na kuitambua, utambulisho wa namba ya mlipakodi, hati ya msawazo na usajili katika mfumo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live