Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trilioni 18 zinapita mitandao ya simu kila mwezi - Serikali

9510add4b596bcb9cd09142c9ef9150c Trilioni 18 zinapita mitandao ya simu kila mwezi - Serikali

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema Sh trilioni 18 zinapita kwenye mitandao ya simu kwa mwezi.

Ndungulile ameyasema hayo alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma jana.

Ndugulile amesema kuwa kiasi cha miamala milioni 300 inafanyika kila mwezi mtandaoni na Serikali inapata Sh bilioni 80 kwa mwezi za tozo zitokanazo na fedha zinazopita mtandaoni.

Aidha amesema kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambayo ndiyo njia kuu ya uchumi, wameweza kusimamia upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuongeza udhibiti na usimamizi wa huduma za mawasiliano kwenye suala la fedha mtandao ili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuweza kuongeza mchango wa tozo Serikalini zaidi ya Sh bilioni 80 kwa mwezi kwa kuwa miamala mingi ya fedha inafanyika na fedha nyingi zinapita kwenye mtandao ili TEHAMA iongeze mchango wake kwenye ukuaji wa uchumi na kuchangia zaidi pato la taifa

Chanzo: habarileo.co.tz