Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Treni ya Dar es Salaam - Moshi kutumia saa 16, TRC yasema ni mwanzo

87352 Pic+tren Treni ya Dar es Salaam - Moshi kutumia saa 16, TRC yasema ni mwanzo

Fri, 6 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati abiria wanaosafiri kutoka Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania wakitutumia saa kumi hadi 11 njiani kufika kwa usafiri wa basi, usafiri wa treni itawalazimu kutumia saa 16.

Usafiri huo wa treni ulisitishwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, unaanza leo Ijumaa Desemba 6, 2019 ambapo Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza ratiba zake.

Kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi itakuwa ni Jumanne na Ijumaa saa 10 jioni na kuwasili Moshi saa 2 asubuhi huku kutoka Moshi kwenda Dar es Salaam itakuwa ni Jumatano na Jumamosi saa 10 jioni na kuwasili Dar es Salaam saa 2 asubuhi.

Kwa ratiba hiyo itamchukua saa 16 njiani abiria atakayepanda usafiri huo.

Mwananchi limezungumza na Mkuu wa kitengo cha habari na uhusiano wa TRC, Jamila Mbarouk kutaka kujua ratiba hiyo inavyoweza kuna kosesha abiria alisema hiyo ni mwanzo tu kwa kuwa ndio wanaanza lakini kadri siku zitakavyokwenda saa hizo zitapungua.

"Muda umekuwa mrefu kwa kuwa ndiyo tunaanza na ukizingatia  njia haijatumika muda mrefu, hivyo hatuwezi kuanza kutembea mwendo wa haraka, lakini  baadaye muda utapungua zaidi," amesema Jamila.

Chanzo: mwananchi.co.tz