Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Treni mpya Dar- Bagamoyo mbioni kuanza

ABIRIA WAKIDANDIA TRENI Treni mpya Dar- Bagamoyo mbioni kuanza

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa ujenzi wa reli ya mjini ili kuimarisha usafiri mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amewaambia wahariri wa habari leo.

Kadogosa amesema mpango wa TRC ni kuwa na treni za kisasa zitakazosaidia watumiaji wa usafiri huo kufika sehemu wanazokwenda kwa wakati. Mpango huo pia utahusisha ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, upembuzi yakinifu umefanyika kwa njia ya Tegeta - Mjini, Mwenge - Bakhresa na Mjini - Mbagala. “Treni zitakazokuja ni mpya na zitakuwa zinatumia dizeli,” Kadogosa aliwaambia wahariri wakati wa semina kwa vyombo vya habari nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live