Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tozo ya miamala yaisababaishia Vodacom kupoteza Tsh bilioni 103.8

Vodacomshop Tozo ya miamala yaisababaishia Vodacom kupoteza Tsh bilioni 103.8

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imesema ilipanga kukusanya Tsh trilioni 1.06 katika mwaka ulioisha Machi 2022 lakini kutokana na athari za Tozo imepoteza 9.8% ya mapato na kukusanya Tsh bilioni 956 ambayo ni pungufu ya hasara ya Tsh bilioni 103.8 ya matarajio.

Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema tozo hizo ziliongeza gharama za wateja kufanya miamala kwa kutumia simu za mkononi, hivyo kusababisha zaidi ya wateja milioni 1.3 kuacha kutumia huduma za M-Pesa.

Kutokana na hali hiyo, huduma ya M-Pesa ambayo imekua namba moja kwa ukusanyaji mapato kwa Vodacom Tanzania, ilishuka kwa 7.6% ya kiasi kilichokusanywa na kampuni hiyo.

Serikali ilianzisha tozo za miamala Juni 2021 ili kutafuta fedha zaidi za ujenzi wa miradi, hata hivyo, utekelezaji wake umepata ukosoaji na kusababisha kushuka kwa miamala ya kifedha kwa njia ya simu huku watu wakitumia njia nyingine mbadala za kutuma na kupokea pesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live