Kampuni ya uzalishaji magari Toyota Motor Corp imesema itasitisha uzalishaji katika viwanda vitano vya ndani kuanzia mwezi Januari.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu inasema kuwa sababu za kusitisha uzalishaji ni kutokana na masuala ya ugavi, uhaba wa chip na janga la COVID-19.
Kampuni kuu ya kutengeneza magari nchini Japani imesema kuwa kusimamishwa kwa viwanda hivyo kutaathiri takriban magari 20,000, lakini hakutaathiri lengo lao la mwaka la kutengeneza magari milioni tisa.
Wiki iliyopita, Toyota ilisema inakadiria punguzo kubwa la uzalishaji wa magari Amerika Kaskazini mnamo Januari hadi vitengo 50,000 kutokana na maswala ya ugavi.