Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tosci kutengeneza lebo mpya kudhibiti mbegu feki

13541 MBEGU+PIC TanzaniaWeb

Fri, 24 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Ili kuongeza uzalishaji wa mazao yatakayotumika kama malighafi kwenye viwanda, taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu nchini (Tosci) iko kwenye hatua za mwisho za kutengeneza lebo mpya itakayowekwa kwenye vifungashio ili kuondoa tatizo la wakulima kuuziwa mbegu feki.

 Hayo  yamesemwa  leo Agosti 23 Mkurugezi Mkuu wa Tosci Patric Ngwediagi wakati wa mkutano wa wataalamu wa taasisi hiyo na Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba uliofanyika kwenye ofisi za taasisi hiyo zilizopo chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo Sua.

 Ngwediagi amesema kuwa lebo hiyo mpya itakuwa na vocha ambayo mkulima atakwangua na kuingiza namba kwenye simu na baadaye kupata majibu kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kama mbegu hiyo ni feki ama imethibitishwa na Tosci.

 Amesema kuwa kama suala la mbegu feki halitadhibitiwa uzalishaji wa mazao utashuka na hivyo mkakati wa Rais John Magufuli wa kuwa na uchumi wa viwanda hautafanikiwa kwa kuwa malighafi nyingi za viwanda zinatokana na mazao ya kilimo.

 Aliongeza kuwa kwa sasa Tosci imeongeza kiasi cha mbegu kilichothibitishwa ubora kutoka tani 10,946 hadi kufikia tani 32,456 hata hivyo ipo changamoto ya uelewa na hamasa ndogo kwa wakulima kuhusu matumizi ya mbegu bora.

Akitaja majukumu ya taasisi hiyo Ngwediagi amesema Tosci imekuwa ikifanya ukaguzi na kusajili kwenye maduka na maghara yanayouza na kuhifadhi mbegu, kufanya majaribio ya utambuzi nay a utambuzi wa mbegu mbalimbali.

 Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba ameitaka Tosci kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwani uwepo wa viwanda unategemea ubora wa mbegu za mazao yatakayotumika kwenye viwanda hivyo kama malighafu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz