Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tochi imulikwe uvuvi ziwa Tanganyika

Uvuvi Ziwa Tanganyika.jpeg Tochi imulikwe uvuvi ziwa Tanganyika

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Habarileo

Wadau wa uvuvi mkoani Kigoma wameiomba serikali kutafakari upya mpango wa kufunga shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika, kwani kutekelezwa kwa mpango huo kutaathiri maisha ya wananchi wa mkoa huo, ambao wanategemea uvuvi kama shughuli yao kuu ya kuwaingizia kipato.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kuwa mpango wa kufunga shughuli za uvuvi ambao ulitangazwa kuanza Mei 15 mwaka huu, unapaswa ufanyiwe tathmini ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa, ili kubaini athari kubwa zitakazojitokeza kwa miezi mitatu ambayo shughuli hizo zitakuwa zimefungwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Manispaa ya Kigoma Ujiji, Ally Kibore alisema kuwa moja ya mambo ambayo wanapinga kutekelezwa kwa mpango huo ni Kanuni zilizowekwa na Mamlaka ya Usimamizi ya Ziwa Tanganyika (LTA), kupitia mradi wa maendeleo ya uvuvi ziwa Tanganyika (LATAFIMA), ambazo zinakwenda tofauti na sheria na kanuni za uvuvi nchini.

Chanzo: Habarileo