Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tira yazitaka kampuni za bima kuwafuata wenye kipato kidogo

75061 Bima+pic

Tue, 10 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania (Tira), Dk Mussa Juma amesema mamlaka hiyo inakusudia kufanya marekebisho ya sheria yake ili kuzibana kampuni za bima kuanzisha bima kwa watu wenye kipato cha chini.  

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita na Mwananchi, Dk Juma alisema kwa sasa kampuni hizo zina wateja wengi wenye kipato cha juu na cha kati, huku wananchi wengi wa kipato cha chini wakikosa huduma.

“Kampuni nyingi za bima zimejikita zaidi katika watu wenye kipato cha kati na cha juu kwa sababu ndiyo wana uwezo wa kulipa. Ukiangalia Watanzania wengi wana kipato kidogo, je ni asilimia ngapi wana bima? Kwa hiyo tuna ‘push’ watu wapate bima,” alisema.  

Alitaja bima hizo kuwa pamoja na bima ya mazao na wafanya biashara ndogo.

“Unakuta kuna kampuni 31, lakini ukiangalia hazina matawi mikoani. Unakuta kampuni iko kwenye mikoa miwili au mitatu. Tunawashawishi ili wawafikie wale wananchi, ndiyo maana tunawashauri wawe na products (bidhaa) nyingi,” alisema.  

Mbali na hilo, Dk Juma alisema Tira inakusudia kurekebisha sheria ili kudhibiti kiwango cha bima kinachouzwa nje ya nchi akisema kwa kufanya hivyo, zinahamisha utajiri kwenda nchi nyingine.

Pia Soma

Advertisement
“Hizi kampuni za hapa nyingi zina uhusiano na kampuni nyingine nje ya nchi, kwa hiyo wanaopeleka kwa kigezo kuwa hawawezi kuretain. Mimi nataka kuwabana asilimia 60 ile inayozidi kwa mfano 40 ndiyo upeleke kwenye bima nyingine,” alisema Dk Juma.  

Kuhusu bima za lazima na zisizo za lazima, Dk Juma alisema wanataka sheria iongeze wigo wa bima za lazima ikiwa pamoja na bima ya nyumba, bima ya afya na bima za ushauri wa kitaalamu.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz