Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu ya IMF yawasili nchini kujadili mkopo wa Tril.2.5

Bot Two Rais Samia Suluhu Hassan alifanya mazungumzo na wakuu wa Benki ya Dunia na IMF

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya wataalamu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) ipo nchini Tanzania kwa ajili ya majadiliano ya mkopo wa Dola za Marekani bilioni 1.1 sawa na Sh2.5 trilioni ambazo Serikali iliziomba hivi karibuni ikiwa ni mwendelezo wa maombi mengine ya mkopo kutoka katika shirika hilo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus amesema kuwa akiwa Marekani mwezi uliopita Rais Samia Suluhu Hassan alifanya mazungumzo na wakuu wa Benki ya Dunia na IMF ambapo Serikali iliomba kupatiwa mikopo.

​Katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Kristalina Georgieva jijini Washington, kiongozi huyo alipokea maombi mengine ya fedha kutoka Tanzania ambapo Serikali imeomba takriban Dola bilioni 1.1.

“Kiasi hicho cha fedha ni sawa Sh2.5 trilioni za mkopo wa masharti nafuu ambazo zikipatikana zitakuwa kwa muda wa miaka mitatu,” Yunus amewaambia wanahabari Jijini Dar es Salaam leo (Mei 12, 2022).

Yunus amesema katika mazungumzo hayo, wataalamu wa pande zote mbili waliambiwa wakamilishe mapema iwezekanavyo.

“Naambiwa timu hiyo imeshafika ipo hapa na ifikapo Alhamisi huenda tukajua majibu yote kama watakubali au la ila inaonekana dalili ni nzuri,” amesema

uzi Waziri wa Nishati January Makamba aliwaambia wabunge kuwa Serikali imeomba mkopo kutoka Benki ya Dunia na IMF utakaosaidia kupunguza maumivu ya kupanda kwa gharama za mafuta nchini.

Hata hivyo, Makamba hakueleza kwa undani kuhusu kiwango cha mkopo huo ulioombwa.

Mei 9 mwaka huu Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ben Mwaipaja alieleza katika taarifa yake kwa wanahabari kuwa timu hiyo ya IMF ipo nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya uchumi na kisera, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa mpango wa shirika hilo wa kuipatia Tanzania mikopo na misaada zaidi ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Tayari IMF ilishaipatia Tanzania mkopo wa Dola za Marekani 567.25 kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa virusi vya Corona (Uviko-19) ambapo pamoja na mambo mengine zilipelekwa katika ujenzi wa shule, maji na kuboresha huduma za afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live