Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiketi za kidigitali na 'hekaheka' zake

A1920f362e772358f1adadc71dfd8f02.jpeg Tiketi za kidigitali na 'hekaheka' zake

Mon, 4 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema itaendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto zitakazojitokeza baada ya kuanza kutumika kwa mfumo wa tiketi za mabasi za kielektroniki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire alisema hayo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema matumizi ya mfumo huo yatampunguzia abiria adha ya kupita kwa mawakala na hivyo kuwa na uhakika na safari yake.

Alikipongeza Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) na wadau wengine wa usafirishaji kwa kutoa ushirikiano kwa kipindi cha miezi mitatu ya majaribio ya mfumo huo na kwamba zoezi hilo likitekelezwa kwa uaminifu litarahisisha shughuli za usafiri kwa wamiliki na abiria kwa ujumla.

“Nichukue fursa hii kuwaomba Taboa na wadau wengine tuen- deleze ushirikiano katika utekelezaji wa mfumo huu wa tiketi kwani manufaa yake yataonekana muda mfupi ujao kwa wamiliki na abiria,” alisema.

Migire alisema utekelezaji wa kazi hiyo ni matokeo ya vikao vya mara kwa mara ambavyo sekta imekuwa ikivifanya na kuwahusisha wadau wote wa usafirishaji lengo likiwa ni kuboresha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo.

Katibu wa Taboa, Priscus Joseph alisema tangu Julai Mosi abiria yeyote anayekata tiketi anaweza kukata popote na kupata tiketi hiyo kwa urahisi. Mfumo wa tiketi za kielektroniki ulianza kutumika Julai Mosi, mwaka huu kwa mabasi yote nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live