Serikali katika Mji Mkongwe na Maarufu kwa Biashara ya Madini ya Vito Chanthaburi nchini Thailand umeiomba Tanzania kufungua milango na kuimarisha ushirikiano kwenye uendelezaji wa Sekta Ndogo ya Madini ya Vito.
Wito huo umekuja baada ya Ujumbe wa Tanzania kuzuru mji huo na kutembelea viwanda vidogo vya kuongeza thamani madini ikiwa ni pamoja na kusanifu madini hayo na kutengeneza bidhaa za urembo.
Biashara ya madini na shughuli za uongezaji thamani madini katika Mji wa Chanthaburi kwa kiasi kikubwa hutegemea malighafi za madini kutoka Tanzania, Nigeria, Madagascar na Msumbiji. Aidha, madini ya Sapphire na Rubi ya Mundarara-Longido ni miongoni mwa madini maarufu katika mji huo.