KAMPUNI ya Tesla imerejesha zaidi ya magari yake ya umeme 475,000 kushughulikia mfumo wa kamera na maswala mengine ya kiufundi ambayo yameonekana kuongeza hatari ya ajali za barabarani, mdhibiti wa usalama barabarani nchini Marekani alitangaza Alhamisi.
Magari yalioathirika na utaratibu huu ni yale yaliyotengenezwa kati ya 2014 na 2021 na jumla ya idadi ya magari yaliyorejeshwa ni karibu sawa na nusu ya magari ambayo Tesla ilitoa mwaka jana.
Watengenezaji hao wa magari ya umeme wanarejesha magari 356,309 mahususi ili kushughulikia dosari ya kamera ya nyuma katika magari yake ya Model 3 toleo la 2017 hadi 2020.
Vile vile magari mengine 119,009 ya Model S yanarejeshwa kutokana na matatizo ya mfumo.