Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Teknolojia ya mawasiliano ni nguzo muhimu ya ukuaji wa biashara nchini

73045 Pic+minara

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam, Imeelezwa kuwa mbali na kuwa mitandao ya simu hutumika kwa mawasiliano lakini pia mitandao hiyo kwa sasa ni nyenzo muhimu kwa wafanyabiashara wa wadogo (SMEs) katika kukuza uchumi na biashara zao kwa ujumla .

Hayo yamo katika repoti iliyotolewa hivi karibuni na taasisi ya GSMA ambapo taarifa hiyo ilisema Sekta hii ambayo inakadiriwa kuwa na wafanyabiashara zaidi milioni tatu nchini kote wanakadiriwa kuchagia zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa (GDP) na kufanya serikali itambue mchango wake hivyo kuiingiza sekta hii kwenye mpango wa taifa wa maendeleo.

Ilisema Mbali na kupiga simu wafanyabiashara hutumia mitandao ya simu kuhifadhi, kutuma na kupokea fedha, kupata huduma bima, kulipia malipo ya vitu na huduma mbalimbali na pia hata huduma kukopa fedha kwa ajili ya miradi au kutatua matatizo yanayowakumba wafanyabiashara wadogo.

“Tunapojadili SMEs ni ukweli usiopingika kuwa sekta ya mawasiliano ni muhimu kwa ukuaji wake. Makampuni ya mawasiliano ya simu hutupatia huduma za vifurushi vya data, kutuwezesha kuwasiliana kibiashara, au na rafiki zetu na familia kwa urahisi na programu tumishi (apps) za makampuni hayo hurahisisha maisha yetu” ilisema taarifa iliyotolewa na GSMA

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa Kutokana na hali hiyo ni muhimu kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua zaidi na zaidi ili wafanyabiashara waendelee kunufaika nayo.

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa msingi wa biashara ni mawasiliano na taarifa kati ya mnunuzi na muuzaji na makampuni ya mawasiliano nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa yanasaidia jumuiya ya wafanyabiashara kukua.

Pia Soma

Taarifa hiyo ilitoa mfano kuwa kupitia kampuni ya Tigo katika huduma yake ya Tigo Pesa kwa sasa watumiaji wake wameungwa na mfumo wa malipo wa serikali (Government’s e-Payment Gateway) na kuwasaidia wafanyabiashara Kurahisisha kulipia ankara zao. Vile Tigo Pesa imewasaidia wafanyabiashara kukusanya malipo ya bidhaa zao.

“Wateja sasa wanaweza kulipia bidhaa zao kwa kutumia programu ya Tigo Pesa au hata kuwalipa wafanyakazi wao. Inakadiriwa kuwa zaidi ya kampuni 70,000 zinatumia huduma za tigo kwa minajili hii,” iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema ili kuoboresha hudma hii, Tigo imezindua njia ya huduma ya online kwa wateja wake kwa kutumia mtandao wa kijamii ujulikanao kama WhatsApp. Huduma hiyo, inawawezesha wateja kuwasiliana na dawati la huduma kwa wateja moja kwa moja na haraka ili kuweza kurahisisha kutatua matatizo ya wafanyabiashara kwa haraka na wakati wowote.

Chanzo: mwananchi.co.tz