Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Teknolojia kutumika kujua idadi ya samaki

75970 Pic+samaki

Tue, 17 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaaam. Nchi tatu za Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi za Tanzania, Kenya na Msumbiji zimeanzisha mradi wa kisasa wa ukusanyaji takwimu za samaki kwa njia ya teknolojia (Fidea) ili kuwa na taarifa za pamoja za kusaidia kulinda na kujua hali ya viumbe hao.

Katika kikao cha pamoja cha kujadili mradi huo wadau kutoka nchi hizo wameshiriki kutoa maoni yao katika mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya Ujerumani.

Mtendaji mkuu wakala wa elimu wa mafunzo ya uvuvi, Yahya Mgawe amesema takwimu hizo zitakusanywa kwa njia ya kiteknolojia katika timu ya wasimamizi wa nchi zote tatu na zitachakatwa na kupata habari zitakazosaidia kufanya uvuvi kuwa endelevu.

"Tulikuwa na ukusanyaji uliozoeleka kabla ila sasa kumetokea mapinduzi makubwa ya kutoa taarifa kiteknolojia, na tunataka takwimu siyo zikusanywe na wanasayansi peke yao bali pia hata wadau kama wavuvi na wote wanaofanya shughuli zinazohusu rasilimali ya uvuvi," amesema Mgawe.

Mgawe ameeleza madhara ya kutokuwa na takwimu za samaki zinapelekea kuisha kwa rasilimali hizo akitolea mfano wa Canada Mashariki ambapo wamezuia shughuli za uvuvi kwa miaka 30 kufuatia uvuvi uliopitiliza na bila ya kuwa na kumbukumbu.

Mgawe ameeleza kuwa Tanzania bado tupo katika hali nzuri ya uvuvi kutokana na usimamizi na ukusanyaji wa takwimu uliokuwepo.

Pia Soma

Advertisement
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri), Dk Semvua Mzighani amesema hatua mbalimbali zinachukuliwa baada ya ukusanyaji wa taarifa ambapo nchini walifungia uvuvi wa kamba (prawns) kuanzia mwaka 2007 hadi 2016 baada ya Tafiri kujiridhisha.

"Jana Septemba 15 watafiti wameenda Ziwa Victoria kufanya utafiti kwenye samaki waliopo. Baada ya Operesheni Sangara hali ya samaki hao imeimarika ukilinganisha na kabla kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka jana, " amesema Mzighani.

"Ili kupunguza nguvu ya uvuaji wa samaki tumeanza kufundisha watu na kuhamasisha kufuga nje ya yale maji ya asili," amesema Mzighani.

Msimamizi wa Mradi wa Ukusanyaji Takwimu za Samaki kwa Ukanda wa Afrika Mashariki (Fidea), Dk Rushingisha George amesema wananchi wa kawaida watanufaika na mradi huo kwa kujua taarifa sahihi za hali halisi ya samaki na hatua zitakazochukuliwa baada ya wao kuwasilisha tafiti zao.

Chanzo: mwananchi.co.tz