Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tawa hutoa asilimia 25 ya mapato kwa mkoa wenye pori la akiba

10796 Tawa+pic TanzaniaWeb

Thu, 5 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa Habari wa Mamlaka ya Wasimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Twaha Twaibu amesema mamlaka hiyo hutoa asilimi 25 ya mapato ya uwindaji na utalii kwa mkoa wenye mapori ya akiba.

Twaha alisema hayo jana katika maonyesho ya kimataifa ya biashara maarufu Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini hapa.

“Mwaka jana Wilaya ya Bariadi, Simiyu walipokea zaidi ya Sh90 milioni zilizoelekezwa katika kusaidia maendeleo ya jamii zinazoishi katika pori la akiba la Maswa,” alisema Twaha.

Alifafanua kuwa banda la wanyamapori kwa mwaka huu katika maonyesho hayo wameongeza wanyama wapya.

Twaha alisema wananchi pia watapata fursa ya kupata habari za uhakika juu ya safari ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi itakayofanyika Agosti 7 na 8 mwaka huu.

Wanyama hao wapya ni choroa, ngedere, tausi, tandala mkubwa na swala ambao wameonekana kuwa kivutio kama walivyo simba na chui.

“Mwaka jana nilikuja kivutio kilikuwa simba, lakini mwaka huu nimevutiwa na tandala mkubwa kwa sababu sijawahi kumuona zaidi ya kwenye maonyesho,”alisema Robert Gabriel.

Chanzo: mwananchi.co.tz