Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tasupa watoa masharti ununuzi wa alizeti Tanzania

Wed, 16 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwenyekiti wa chama cha wasindikaji mafuta alizeti Tanzania(Tasupa)  Ringo Iringo amewataka wakulima wa zao hilo kuacha kutumia mbegu za kienyeji ambazo hazina ubora kwani msimu ujao hawatanunua alizeti iliyozalishwa kwa mbegu za kienyeji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, leo Jumanne Oktoba 15,2019, Iringo amesema tahadhari hiyo ni kufuatia wakulima wengi kutumia mbegu za kienyeji msimu uliopita ambazo hazina ubora wowote katika zao hilo.

Amesema wakulima wanatakiwa kutumia mbegu bora ili kufanya mafuta  kuwa mengi na kuepusha hasara kwa mkulima pamoja na msindikaji hivyo.

Amesema maofisa kilimo wanatakiwa kuwaelimisha wakulima kuhusu matumizi ya mbegu bora.

“Kuelekea msimu wa kilimo, Desemba hadi Februari mwakani tunajua ndio msimu wa kilimo na inavunwa kati ya siku 105 hadi 120 sasa tumeamua kutoa ushauri huu kwa wakulima kuhusu matumizi ya mbegu bora,”  amesema Iringo

“Kumekuwa na tabia ya wakulima kurudia mbegu zile zile kila wakati mbegu ambazo zimeshashuka ubora, hii inamfanya mkulima kupata mazao kidogo, kwa msindikaji ananunua magunia mengi halafu akikamua alizeti anapata mafuta kidogo, sasa hasara hii hatuitaki na tunasema kuwa hatutanunua alizeti inayotokana na mbegu za kienyeji,” amesema

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz