Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tasupa wataja changamoto uzalishaji wa alizeti

32493 Alizetipic Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwenyekiti wa taasisi ya wazalishaji wa mafuta ya alizeti  nchini (Tasupa),  Ringo Iringo amesema uzalishaji wa mafuta ya alizeti unakabiliwa na changamoto inayorudisha nyuma  maendeleo yao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 19, 2018 mjini Dodoma katika warsha ya kujadili mafanikio waliyoyapata baada ya Serikali kuongeza ushuru wa forodha wa asilimia 25 kwenye mafuta ghafi ya kula.

Katika hafla hiyo pia walizindua ripoti yenye takwimu zinazoonyesha hali halisi ya sekta ya mafuta ya kula nchini Tanzania.

Amesema kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mashudu pamoja kodi kwenye viwanda vinavyozalisha mafuta ya alizeti kunasababisha kusiwe na ushindani wa soko la mafuta kutoka nje.

Amesema kuna kodi nyingine takribani 65 zinakwamisha sekta ya uzalishaji wa mafuta nchini na kuiomba Serikali kuzipitia upya kodi hizo ili kumpunguzia mwananchi mzigo wa kodi.

Hata hivyo amesema kuna mafanikio baada ya Serikali kuongeza ushuru wa forodha kwenye mafuta ghafi kutoka nje kutoka asilimia 10 hadi 25 kwa kuwa bei ya alizeti kwa sasa imeongezeka kutoka Sh450 hadi Sh700 hadi Sh850  na Sh1,050 kwa kilo.

“Pia kumekuwa na ongezeko kubwa la viwanda vya kusafisha mafuta ya alizeti vikubwa na vidogo. Vilikuwa 12 mwaka 2017 ila kwa sasa vimefikia viwanda 25. Hii inatokana na Serikali kupandisha ushuru wa forodha kwa mafuta ghafi,” amesema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz