Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarura kujenga barabara, madaraja 269

Barabara Madaraja Tarura kujenga barabara, madaraja 269

Sun, 14 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amesema kwa mwaka wa Fedha wa 2022/22 Tarura itajenga barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 422, kiwango cha changarawe urefu wa kilometa 11,074 huku madaraja 269 yakijengwa.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo Jumapili Agosti 14, 2022 wakati wa utiaji saini mikataba kati ya Tarura na makandarasi watakaotengeneza kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo hafla hiyo iliyofanyika jijini Dodoma mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema bajeti ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara vijijini na mijini imeongezeka kutoka Sh272.56 bilioni mwaka 2020/21 hadi Sh722 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 185.

Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati ambapo Tarura imetengewa bajeti ya jumla ya Sh838.16 bilioni ambapo kati ya hizo Sh776.63 bilioni ni fedha za ndani na Sh61.53 bilioni ni fedha za nje.

Amesema Tamisemi ilitoa maelekezo kwa Tarura kuanza taratibu za manunuzi mapema ili kazi ziweze kuanza kabla ya kipindi cha mvua ambapo tayali Tarura ilitangaza zabuni 1,085 zenye thamani ya Sh378.56 bilioni, sawa na asilimia 60% ya fedha zilizopangwa kutekeleza miradi ya barabara za vijijini na mijini, kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Bashungwa amesema mpaka sasa miradi iliyotayari kusainiwa ni mikataba 968, yenye thamani ya Sh248.74 bilioni, na miradi yenye thamani ya Sh129.83 bilioni, imetangazwa upya baada ya makandarasi walioomba kutokidhi vigezo.

Waziri huyo amesema kupitia Mradi Agriconnect kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU), barabara zenye urefu wa kilomita 65 kwa kiwango cha lami zitajengwa kwa gharama ya Sh37.6 bilioni.

Pia, amebainisha kuwa mwaka 2021/22, Serikali iliweza kuajiri wahandisi 255, ambao kati ya hao wahandisi 185 walielekezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo unapeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya halmashauri, wahandisi 56 walielekezwa katika Sekretarieti za Mikoa, ambazo zina jukumu la ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, na wahandisi 14 walielekezwa Tarura.

Ameeleza katika mwaka wa fedha 2021/2022 yaliagiza magari 130 kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya barabara, na tayari yameshapokelewa magari 4, na wanaendelea kufuatilia upatikanaji wa magari 126 ambayo hayajapokelewa.

Waziri huyo wa Tamisemi ametoa wito kwa makandarasi pale wanapofanya kazi katika maeneo mbalimbali katika halmashauri kutimiza  jukumu lao la kulipa kodi husika (Service Levy) na wanapoandaa zabuni zao wakumbuke sehemu ya kodi ambazo huchangia kwenye mapato ya halmashauri zinazopaswa kulipwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live