Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taratibu upimaji udongo zipo hivi...

Ed189f7286b30a56d0906b7b36ef4514 Taratibu upimaji udongo zipo hivi...

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima kutoka maeneo mbalimbali wamepata elimu zinazohusisha teknolojia bora za kilimo pamoja na upimaji wa udongo kwa kilimo chenye tija.

Mkulima Magreth Kikoti kutoka Halmashauri ya Mufindi mkoani Iringa, ni miongoni mwa wakulima wengi waliokuwa na shauku ya kujifunza jinsi ya kupima udongo katika banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), lililopo katika maonesho ya Nanenane Viwanja vya John Mwakangale, Mbeya.

Alisema amefika kujifunza katika taasisi hiyo, kwa kuwa kwa kushirikiana na wana kikundi wenzake, wamekusudia kuzalisha mbegu za viazi na maharage kabla ya msimu wa kilimo kufika.

Alisema anataka kujua anapaswa kutumia mbolea ya aina gani, virutubisho vipi vimepungua kwenye udongo katika shamba walilonalo.

Naye Mkurugenzi wa TARI Mlingano, Dk. Catherine Senkoro, alisema wakulima wengi wa Nyanda za Juu Kusini, ambao wanatumia mbolea kila msimu bila kupima afya ya udongo, wamekuwa hawajui kiasi ambacho kinahitajika cha virutubisho, kulingana na aina ya zao ikilinganishwa na afya ya udongo.

“Kwa sababu hiyo wanaweza wakawa wanapoteza fedha kuweka virutubisho, ambavyo tayari vinatosha. Kama wanaongeza mbolea bila kupima wanaweza wakawa wanachafua mazingira, ikiwa ni pamoja na afya ya udongo,” alisema.

Alisema virutubisho vingine ni sumu kama vitazidishwa na kutolea mfano wa nitrojen, ambayo alisema inaweza kuharibu maji yaliyoko ardhini, lakini mkulima akipima afya ya udongo, atajua aina ipi inatakiwa iwepo, na kwa kiasi gani italeta tija na kutunza mazingira.

“Ili kufikia asilimia 10 ifikapo 2030, haya yanapaswa kufanyika, kwa sababu afya ya udongo ni muhimu katika kuleta tija katika kilimo,” alisema.

Alisema Nyanda za Juu Kusini wamepima na kugundua kuna tindikali, ambayo ambapo mkulima anapaswa kutumia mbolea na chokaa mazao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live