Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Mwanzilishi wa Red Bull afariki Dunia

Red Bull .jpeg Mwanzilishi wa Red Bull afariki Dunia

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanzilishi na Mmiliki wa Kampuni ya Red Bull, Bilionea Dietrich Mateschitz, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mateschitz (78) Mfanyabiashara maarufu duniani kutokea Austria anatajwa kuwa mtu tajiri kuliko wote nchini humo, ambaye alifanikiwa kujenga jina kubwa kwa kinywaji cha Red Bull.

Bilionea huyo pia ni mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya Mashindano ya magari ya Formula 1 iitwayo Red Bull Racing.

Uongozi wa Formula 1 umemsifu kwa mchango wake mkubwa kwenye mchezo huo na kusema kuwa ameacha alama ambayo haitofutika.

Maisha binafsi ya bilionea huyo aliyekuwa akiishi katika mji wa Salzburg hayakuweza kujulikana kirahisi, alikuwa mkimya na hakupenda kuhojiwa, aliwahi kusema kuwa alikuwa akinywa makopo 10 hadi 12 ya Red Bull kwa siku miaka ya nyuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live