Mtwara. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema mkoa huo umetenga eneo la zaidi ya ekari 2,000 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya korosho.
Amesema eneo hilo ni kwa wawekezaji watakaovutiwa kuwekeza mkoani humo.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 12, 2019 katika kongamano la kimataifa la uwekezaji katika sekta ya ubanguaji wa korosho lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) linalofanyika mkoani Mtwara na kujumuisha kutoka nchi 10.
Zambi amesema wamedhamiria kuongeza uzalishaji wa korosho na wanawaalika wawekezaji kuwekeza katika viwanda ili kulinda ajira na bidhaa nyingine zinazotokana na korosho kuzalishwa nchini.
Amewahakikishia amani na usalama nchini na watakaoweza wawe na uhakika mali watakazowekeza hazitapotea.
Amesema mkoa huo ulikuwa ukizalisha korosho kwa kiasi kidogo lakini kwa miaka miwili uzalishaji ulianza kuongezeka kutokana na jitihada za serikali wanatenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na ndani ya miaka mitatu wameweza kusambaza miche mipya ya korosho zaidi ya milioni 7.
Pia Soma
- Gari la ‘mahakama inayotembea’ lazinduliwa Mwanza
- Haya ndiyo maajabu ya shule ya Kibaha
- Rais Museveni kumtembelea Magufuli Chato