Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yawakaribisha wadau kutoka Ubelgiji

Mkumbo Biz Prof. Kitila Mkumbo.

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imewaalika wawekezaji kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza nchini ikieleza kuwa uwekezaji huo hauwezi kuwa wa gharama kubwa kama ilivyo katika nchi zilizo endelea.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema katika Mkutano wa Jumuiya hiyo unaojadili upatikanaji wa Madini adimu (Critical Minerals ) huko Brussels nchini Ubelgiji kuwa hakuna haja ya kuhofia kuwekeza katika mataifa ya Afrika.

“Kuna idadi kubwa ya rafiki zetu kutoka upande wenu (Magharibi), ambao bado wanafikiri kuwa ni vigumu na ghali kuwekeza viwanda vya uchakataji na uongezaji thamani wa madini adimu Afrika na Tanzania, ninawaambia kila vilivyo vizuri ni ghali, ni vigumu lakini vinawezekana, ninawakaribisha kuwekeza Tanzania na mtafurahi”, alisema Prof. Mkumbo.

Alisisitiza wadau wa maendeleo wa nchi za Jumuiya ya Ulaya na washiriki wa Mkutano huo kuwa ni vyema wakaondoa hofu za kimtazamo kwamba, uwekezaji wa viwanda vya uchakataji wa madini adimu ni ghali kufanyika Afrika ukilinganisha na Ulaya.

Prof. Mkumbo amesema kuwa Tanzania ina sehemu muhimu katika kufanikisha agenda ya dunia katika kuyafikia mabadiliko ya matumizi ya nishati ya kijani kwani imejaaliwa kuwa na rasilimali zinazohitajika.

Katika mchango wake Waziri huyo mwenye dhamana ya Mipango na Uwekezaji nchini amesisitiza kuwa Tanzania ina Sera zilizo wazi zinazolenga kujenga uchumi shindani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live