Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yauza tani 10,000 za nyama Bara la Asia

NYAMA 1 Tanzania yauza tani 10,000 za nyama Bara la Asia

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema katika kipindi cha miezi sita Tanzania imeuza nyama tani 10,000 katika nchi za Bara la Asia tofauti na miaka ya nyuma.

Waziri Ndaki ameyasema hayo jana Julai 4 wakati ya akifungua warsha ya siku saba ya wataalamu wa sekta ya mifugo kutoka  nchi za  Jumuiya  ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili namna ya kuongeza thamani ya nyama nyekundu yanayotokana na ng'ombe wa asili.

Amesema ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchini za Bara la Asia hususani nchi za Kiarabu zimefungua mwanga wa masoko, ambapo hadi Desemba mwaka huu huenda Tanzania ikauza nyama nyingi kuliko miaka yote.

Waziri Ndaki amesema kuwa, kutokana na hilo kupitia Wizara yake wamepanga mpango kazi wa kuhakikisha wanafuga mifugo bora yenye lengo la kumpatia mlaji bidhaa bora kwa maslahi ya nchi.

"Katika kipindi cha mwaka jana, Tanzania iliuza nje ya nchi nyama tani 7,000 lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti sana kwani katika kipindi cha miezi sita nchi imefanikiwa kuuza nje ya nchi nyama tani 10, 000," amesema Waziri Ndaki.

 Waziri Mashimba ameongeza kuwa serikali imepanga kushirikiana na nchi za SADC katika kuboresha mifugo na kuwa na nyama bora kwa masoko ya kimataifa, kwani nchi hizo zina mifugo bora zaidi.

Kwa upande wake mtaalamu wa teknolojia, ujuzi na ubunifu katika mradi wa Live2Afrika (AU-IBAR), Dk Mary Kariuki amesema kuwa, wamekuwa na mijadala ya kutosha katika eneo hilo katika kuhakikisha wanaboresha mnyororo wa thamani ya nyama katika ukanda wa SADC.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Muungano wa Afrika kwa rasilimali za Wanyama(AU -IBAR), Dk Nick Mwankpa amesema wataalamu wa nchi hizo watatoka na maazimio yenye tija kwa nchi hizo na kwenda kufanyiwa kazi kwa ajili ya faida ya nchi hizo na sio vinginevyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live