Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yashiriki mkutano wa mwaka AfDB

Philip Mpango Tanzania yashiriki mkutano wa mwaka AfDB

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango yupo nchini Misri, ambapo anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Mkutano huo unajumuisha mkutano wa mwaka wa Baraza Kuu la Benki ya Maendeleo ya Afrika na Mkutano wa 49 wa Mfuko wa Maendeleo ya Afrika.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utajadili namna Afrika inavyoweza kutumia sekta binafsi katika kutekeleza ajenda ya mabadiliko ya Tabianchi ili kufanikisha lengo lake la maendeleo jumuishi ya kijani.

Mkutano huo unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali, Mawaziri wa Fedha, Magavana, Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Sekta Binafsi pamoja na Wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live