Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yashiriki maonesho ya kimataifa ya kahawa

Kahawa Web Tanzania yashiriki maonesho ya kimataifa ya kahawa

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Tanzania imeshiriki Maoneshoya Kimataifa ya Kahawa Japan yanayojulikana 2022 Japan Specialty Coffee Conference &Exhibition yaliyoanza tarehe 12 Oktoba 2022 na kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba 2022 jijini Tokyo, Japan.

Maonesho haya ya kimataifa ya kahawa Japan yameandaliwa na Taasisi ya Kahawa ya Japan (SpecialtyCoffee Association of Japan – SCAJ) na kushirikisha makampuni na taasisi sizinazohusika na kahawa zipatazo  235  kutoka nchi zinazozalisha kahawa duniani.

Bodi ya Kahawa Tanzania (Tanzania Coffee Board) imeshiriki pamoja na wawakilishi vyama viwili vya ushirika na makampuni matatu ya Kitanzania yanayohusika na uzalishaji na uuzaji wa kahawa yakiwemo, Kagera Cooperative Union (KCU),Karagwe District Cooperative Union (KDCU), Kampuni ya Kaderes Peasants Development (KPD), Kampuni ya Acaciana Kampuni ya Touton Tanzania Ltd.

Makampuni ya Japan yameonesha kuvutiwa na kahawa ya Tanzania na kuanza hatua za awali za manunuzi ya kahawa hiyo yenye umaarufu nchini Japan.

Hii ni fursa adhimu katika kukuza soko la kahawa ya Tanzania nchini Japan ambayo ni kahawa pendwa Japan iliyopewa jina maarufu la kibiasharala “Tanzania Kilimanjaro Coffee”.

Chanzo: Eatv