Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yashiriki maonesho ya kimataifa ya Utalii duniani

Tz Utalii.jpeg Baadhi ya washiriki wakipata maelezo kwenye banda la Tanzania katika maonesho hayo

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania inashiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii (FITUR) yanayofanyika katika ukumbi wa IFEMA mjini Madrid, Uhispania.

Tanzania inawakilishwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa wenye kuwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia katika Falme ya Uhispania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (United Nations World Tourism Organisation), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Eneo la Hifadhi la Ngorongoro (NCCA), Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Mamlaka ya Huduma za Misitu (TFS).

Lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi washiriki ili kuinua sekta ya utalii.Maonyesho hayo yalifunguliwa tarehe 19 Januari 2022, na Mfalme Felipe VI, ambayo yatahitimishwa tarehe 24 Januari 2022. Banda la Tanzania limekuwa kivutio kwa kutembelewa na wageni wengi ambao wameonyesha nia ya kutembelea Tanzania bara na visiwani. Maonyesho hayo yanashirikisha nchi zaidi ya 160 na kuhudhuriwa na mawaziri kadhaa wa Utalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live