Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yasaini mkataba wa ulinzi wa "Haki Miliki" za wasanii-wabunifu

Brela Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa

Sat, 21 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NCHI Wanachama wa Shirika la Kanda ya Afrika la Miliki Ubunifu (ARIPO) wamekutana Nchini Uganda kujadili masuala ya miliki bunifu kwa upande wa Kanda ya Afrika.

Mkutano huo mkuu wa siku tisa uliofunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Uganda, Kiryowa Kiwanuka unafanyika katika hoteli ya Munyonyo jijini Kampala.

Kiwanuka, amesisitiza ushiriki wa nchi wanachama kujadili kwa kina itifaki hii ili iongeze tija na ufanisi kwa nchi wanachama kwenye kulinda wasanii na kazi zao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa amesema washiriki watajadili na kupitisha Itifaki ya Usajili na Ulinzi wa Hiari wa Haki Miliki kama itaridhiwa na Mawaziri wa nchi wanachama.

"Kwa nchi ya Tanzania, utiaji saini wa Itifaki hii itasaidia wasanii kusajili na kupata ulinzi wa kazi zao nje ya nchi wanachama ambapo ni tofauti na ilivyo sasa msanii akisajili ARIPO anaweza kuomba ulinzi nchi mbalimbali", ameeleza Nyaisa.

Nyaisa, ameongeza Itifaki hiyo itasainiwa na Mawaziri wa nchi wanachama wa ARIPO Agosti 27 na 28, 2021 baada ya kuijadili kwa kina.

BRELA ni taasisi inayosimamia masuala ya Miliki Ubunifu ambayo ni nyanja inayohusu uwezo wa ubunifu wa mtu au watu katika kuunda vitu au kutoa huduma.Inahusisha masuala ya hataza, tunzi, fasihi na kazi za sanaa, alama kwenye bidhaa na huduma, maumbo ya mikebe ya bidhaa na nyinginezo.

Pia inahusu uwezo wa ubunifu wa binadamu unaotambuliwa chini ya mfumo wa Sheria wa Ulinzi wa Bunifu mbalimbali.Mbali ya ushiriki wa BRELA washiriki wengine kutoka Tanzania ni Wizara ya Viwanda na Biashara na Chama cha HakiMiliki Tanzania (COSOTA).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live