Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yasaini mikataba 19 ya nchi na nchi

ContractLaw Tanzania yasaini mikataba 19 ya nchi na nchi

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: mwanachidigital

Imeelezwa kuwa Tanzania imesaini mikataba 19 ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT) hadi kufikia mwaka 2022, ambayo baadhi yake bado haijaridhiwa.

Akizungumza leo Agosti 02, 2023 katika mjadala wa Twitter space ulioendeshwa na Mwananchi, Mhariri wa Takwimu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Halili Letea amesema Tanzania ina mikataba ya aina hiyo kwa lengo la kumlinda mwekezaji.

Mjadala huo umebeba mada ya ‘Je kuna tija yoyote kwa Tanzania kuendelea na mikataba ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT)?’

Halili ametoa mfano wa mikataba iliyoingiwa na nchi ya Afrika Kusini uliongiwa mwaka 2005, Tanzania na Canada 2013, Misri na Tanzania 1997 na mingine.

“Mikataba ya aina hii inakuwepo kulinda maslahi ya mitaji ya wawekezaji. Hadi 2022 Tanzania ilikuwa na mikataba ya aina hii 19, mfano wa mikataba hii ni ule wa kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliongiwa mwaka 2005,”amesema

Katika maelezo yake kupitia mjadala huo, Letea amesema wakati mwingine makubaliano hayo huvunjwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya sheria na utashi wa kisiasa.

“Historia ya mikataba hii ilianza mwaka 1959 ambayo ilianza kati ya nchi ya Ujerumani na Pakistani. Asilimia 96 ya mikataba ya aina hii ilihuisha nchi za Ulaya na nchi maskini, tunaweza kujiuliza hii kwa nini ilitokea hivi?” amesema.

Amesema hadi kufikia mwaka 2016 mikataba hiyo ilifika 3,324 ikihusisha nchi zilizoendelea na maskini.

“Tunaweza kujiuliza je, ni kweli mikataba ya aina hii inavutia uwekezaji? Tunaendelea kujiuliza je Tanzania inanufaika na mikataba ya aina hii,”amehoji.

Chanzo: mwanachidigital