Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaruhusu usafirishaji wa wanyamapori nje ya nchi

Wanyaporipic Data Tanzania yaruhusu usafirishaji wa wanyamapori nje ya nchi

Sun, 5 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 4, 2022 na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, imesema ruhusa hiyo ni kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5, 2022.

“Ili kufanikisha zoezi hili, wafanyabiashara wenye wanyamapori waliosalia kutokana na biashara ya wanyamapori hai na ambao wamefanyiwa uhakiki wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zote muhimu katika Ofisi za Utalii na Huduma za Biashara zilizopo jijini Arusha.

“Usafirishaji wa wanyamapori hao utafanyika kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wadau watakaoruhusiwa kusafirisha wanyamapori ni wale wenye leseni ya biashara ya Nyara (TDL) zilizohuishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live