Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yapepea utekelezaji agenda ya 2063

Tulinde Vyanzo Vya Maji Kwa Wivu Mkubwa   Biteko Tanzania yapepea utekelezaji agenda ya 2063

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye utekelezaji wa makubaliano ya Ajenda 2063, ya kuifanya Afrika kuwa mahali pa ndoto yetu kuelekea Afrika tuitakayo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko kwenye Mkutano wa kujadili utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na Wakuu wa Nchi juu ya Ajenda 2063 kwa nchi za Afrika, alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo jijini Gaborone, Botswana, ulioenda sambamba na maadhimisho ya Tamasha la KUSI.

Dk Biteko alisema kuwa, kimsingi Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ajenda hiyo ikiwemo masuala ya amani, usalama na demokrasia kupewa kipaumbele kwenye nchi, kuunganisha miradi mbalimbali ya maendeleo na nchi za Afrika ikiwemo ule wa SGR, pamoja na miradi ya umeme kupitia nchi za Kenya, Uganda, Ethiopia, na Zambia, na kufungua fursa za kiuchumi kwa nchi za Afrika.

"Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika itaendelea kutekeleza, kusimamia,na kuendeleza harakati hizi za kuifanya Ajenda hii kutimiza Dira ya Afrika tuitakayo. "Alisisitiza Dk.Biteko.

Ajenda ya Afrika 2063 Afrika tuitakayo imebeba vipaumbele saba ambavyo ni pamoja na kuleta Afrika pamoja kwenye masuala ya Maendeleo, kuunganisha Bara la Afrika kwenye masuala ya kisiasa kwa kutumia tunu za Afrika, Utawala Bora na unaozingatia sheria, demokrasia, na haki, kuilinda Afrika, Afrika yenye mwelekeo wa utamaduni wake na maadili, Afrika itakayowaletea maendeleo watu wake, kwa manufaa ya wanachi wa Afrika.

Aidha Dk. Biteko alishiriki mjadala wa Marais kutoka Afrika kuhusu Ajenda ya umoja wa Afrika 2063 ijulikanayo kama Africas Agenda 2063 inayotoa mwelekeo wa Afrika kutimiza ndoto zake na kuifanya Afrika waitakayo. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live