Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaongoza kuuza Korosho yenye ubora

Korosho.png Tanzania yaongoza kuuza Korosho yenye ubora

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho nchini Francis Alfred amesema Tanzania ni nchi pekee inayouza Korosho zake nje ya nchi ikiwa na viwango vya ubora vinavyotakiwa kwa soko la Dunia

Akizungumza Jiiini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Francis Alfred amesema ubora huo wa Korosho umeiweka nchi ya Tanzania kuwa ya 5 kidunia kati ya nchi 46 hali inayochangia kwa kiwango kikubwa kuliingizia taifa fedha za kigeni nakuongeza ushindani kibiashara.

Katika hatua nyingine Francis amesema ili Tanzania iweze kuwa na soko la uhakika na endelevu ni lazima Korosho ziuzwe zikiwa zimebanguliwa na sio Korosho ghafi ili kuongeza soko kimataifa kwa kwa nchi kama Marekani ,Ulaya, Mashariki ya Kati,China ,Uarabuni na South Afrika kwani kwa sasa Korosho nyingi kutoka Tanzania zinauzwa India na Vietnam tu kwasababu hao ndio wenye viwanda vya kubangua kwaua wanauza Korosho ghafi.

Alisema Tanzania mpaka sasa inaviwanda vya Korosho 52 na viwanda vyenye mitambo inayofanya kazi ni takribani viwanda 22 mpaka 30 na vinauwezo wa kubangua tangu Elfu Sitini na nne na mia tano kwa mwaka na vile viwanda ambavyo havijawekewa mitambo kama vikiwekwa mitambo inayofanya kazi vizuri na kubangua Korosho ni wazo Tanzania itaweza kubangua zaidi ya tani laki moja na themanini na tano kwa mwaka.

Tarehe 14 October 2022 wamepanga kuanza minada ya Korosho na mwaka huu wamepanga kuzalisha tani laki nne za Korosho na mfumo watakaotumia ni mfumo wa stakabadhi gharani kwakua bado hali ya soko ulimwengenu ni nzuri hivyo wakulima watapata dhamani ya mazao yao huku akiwataka wakulima na vyama vya msingi kuanza kukusanya Korosho nakuzipeleka gharani kusubi soko kwani mwaka huu 2022 wanahitaji magunia milioni tano kwakua tayari wanamagunia na vifungashio vinavyoweza kuweka tani laki tatu na arobaini na tano na wameshayasambaza yakiwa na nembo yenye alama ya eneo zinapotoka Korosho ya chana kikuu na alama ya chama cha msingi ili kubaini kila Korosho zinapotoka na pindi litokeapo tatizo iwe rahisi kwao kujua zilipotoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live