Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yang'ara mafunzo ya anga kidunia

ATCL ATCL CARGO TWO.jpeg Tanzania yang'ara mafunzo ya anga kidunia

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHUO cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ni miongoni mwa vitivo 35 pekee kati ya nchi 195 ulimwenguni kuidhinishwa na kupata ithibati ya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), ili kutoa mafunzo ya usalama wa usafiri wa anga. Chuo hiko pia ni kati ya vyuo tisa tu Afrika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari katika Mkutano wa Sita wa Baraza la Wafanyakazi wa TCAA, alipokuwa akizungumzia hatua zilizopigwa na TCAA kwa miongo miwili ya utendaji kazi wake ndani ya nchi hata kimataifa, katika ofisi za Makao Makuu, Banana, Dar es Salaam.

"Hatua hii inaenda sambamba na kufunguka kwa fursa mbalimbali ikiwemo kupokea wanafunzi wa nje ya nchi. Kuongezeka kwa idadi ya wakufunzi watakaotoa mafunzo," amesema Johari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live