Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yanadi madini kimataifa

Madini Pic Data Tanzania yanadi madini kimataifa

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Madini imetumia fursa ya Maonesho ya 68 ya Vito na Usonara yanayoendelea jijini Bangkok nchini Thailand’ kuhamasisha fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini nchini.

Katika kutekeleza hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amefanya mahojiano na mwakilishi wa jarida la kimataifa la kuchapisha na kutangaza masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini duniani la The New Jeweller, Anand Parameswaran.

Pamoja na masuala mengi yaliyozungumzwa, Mbibo amemueleza Parameswaran mambo kadhaa ikiwemo mazingira wezeshi ya kibiashara katika Sekta ya Madini ambayo yamekuwa moja ya kichocheo kikubwa kinachopelekea wawekezaji wakubwa kuichagua Tanzania.

Pia Mbibo amemweleza kwamba, Serikali imekuwa ikizifanyia kazi kwa karibu changamoto na mapungufu ambayo yameonekana kuwa kikwazo katika biashara ya madini ambapo imewezesha kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Madini na Kanuni mbalimbali zinazosimamia Sekta ya madini nchini.

Kupitia mahojiano hayo, Mbibo amewaalika wadau mbalimbali kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini linalotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26, 2023 jijini Dar es salaam.

Tanzania imekuwa kivutio katika maonesho hayo ambapo inatajwa kwa sehemu kubwa ya madini ya vito yanayopatikana kwenye maonesho hayo yana asili ya Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live